Thursday 28 April 2022

Wanafunzi Wa Kidato Cha Kwanza Sasa Kuripoti Shuleni Mei 4 Badala Ya Mei 3

17:10 By



Picha (Getty images).

NA CHARLES WASONGA

WIZARA ya Elimu imeahirisha tarehe ambayo wanafunzi wa kidato cha kwanza wanatarajiwa kuripoti katika shule za upili walizoitwa kujiunga nazo.

Katika taarifa iliyotumiwa walimu wakuu wa shule za upili na Chama cha Kitaifa cha Wazazi (NPA), Katibu wa Elimu Julius Jwan alisema kuwa wanafunzi hao sasa wataripoti shuleni mnamo Jumatano, Mei 4, 2022.

Awali, wanafunzi hao ambao walipokea matokeo yao ya mitihani wa kitaifa wa darasa la nane (KCPE) mapema mwezi jana, waliratibiwa kuripoti shuleni mnamo Mei 3, 2022.

Tarehe hiyo sasa imebadilishwa baada ya Mei 3, kutangazwa katika siku ya mapumziko kutoa nafasi kwa Waislamu kusherehekea Siku Kuu ya Idd-ul-Fitr.

Siku Kuu hii ni ya kuadhamisha mwisho wa mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

“Waziri wa Masuala ya Ndani Fred Matiang’i ametangaza rasmi Mei 3, kuwa siku ya mapumziko, siku ambayo wanafunzi wa kidato cha kwanza walitarajiwa kuripoti shuleni.

“Kwa sababu hiyo imeamulikwa kwamba siku ya wanafunzi hao kuripoti itakuwa Alhamisi, Mei 4, 2022. Tafadhali hakikisha kuwa mabadiliko haya yanazingatiwa,” Dkt Jwan akasema katika taarifa hiyo.

0 comments:

Post a Comment