Thursday 28 April 2022

KIVUKO CHA MV.PALMA CHA ZINDULIWA RASMI MWANZA

17:17 By


Serikali ya mkoa wa Mwanza jana Aprili 27 imezindua rasmi kivuko kipya cha MV. Palm mali ya Serikali ya Uganda kilichojengwa na kampuni ya kitanzania ya Songoro marine ya jijini Mwanza.

Kivuko hicho chenye uwezo wa kubeba abiria 500, gari kubwa 34 na gari ndogo nne, kimegharimu zaidi ya shilingi Bilioni 7, ambacho pia ni kivuko kikubwa kuliko vyote nchini Uganda.

Akizungumza mbele ya mkuu wa mkoa wa Mwanza, Mhandisi Robert Gabriel, Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo Major Songoro, amesema walipata zabuni ya kutengeneza kivuko hicho mwaka 2018 baada ya kuwabwaga washindani wao kutoka mataifa mbalimbali duniani.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Mhandisi Robert Gabriel, pamoja na kuzitaka nchi nyingine kuja Tanzania kutengeneza Meli na vivuko lakini akaeleza, Serikali itaendelea kulinda wawekezaji na kuwatengenezea mazingira rafiki ya uwekezaji.

0 comments:

Post a Comment