Thursday 28 April 2022

KIVUKO CHA MV.PALMA CHA ZINDULIWA RASMI MWANZA

17:17 By


Serikali ya mkoa wa Mwanza jana Aprili 27 imezindua rasmi kivuko kipya cha MV. Palm mali ya Serikali ya Uganda kilichojengwa na kampuni ya kitanzania ya Songoro marine ya jijini Mwanza.

Kivuko hicho chenye uwezo wa kubeba abiria 500, gari kubwa 34 na gari ndogo nne, kimegharimu zaidi ya shilingi Bilioni 7, ambacho pia ni kivuko kikubwa kuliko vyote nchini Uganda.

Akizungumza mbele ya mkuu wa mkoa wa Mwanza, Mhandisi Robert Gabriel, Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo Major Songoro, amesema walipata zabuni ya kutengeneza kivuko hicho mwaka 2018 baada ya kuwabwaga washindani wao kutoka mataifa mbalimbali duniani.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Mhandisi Robert Gabriel, pamoja na kuzitaka nchi nyingine kuja Tanzania kutengeneza Meli na vivuko lakini akaeleza, Serikali itaendelea kulinda wawekezaji na kuwatengenezea mazingira rafiki ya uwekezaji.

Wanafunzi Wa Kidato Cha Kwanza Sasa Kuripoti Shuleni Mei 4 Badala Ya Mei 3

17:10 By



Picha (Getty images).

NA CHARLES WASONGA

WIZARA ya Elimu imeahirisha tarehe ambayo wanafunzi wa kidato cha kwanza wanatarajiwa kuripoti katika shule za upili walizoitwa kujiunga nazo.

Katika taarifa iliyotumiwa walimu wakuu wa shule za upili na Chama cha Kitaifa cha Wazazi (NPA), Katibu wa Elimu Julius Jwan alisema kuwa wanafunzi hao sasa wataripoti shuleni mnamo Jumatano, Mei 4, 2022.

Awali, wanafunzi hao ambao walipokea matokeo yao ya mitihani wa kitaifa wa darasa la nane (KCPE) mapema mwezi jana, waliratibiwa kuripoti shuleni mnamo Mei 3, 2022.

Tarehe hiyo sasa imebadilishwa baada ya Mei 3, kutangazwa katika siku ya mapumziko kutoa nafasi kwa Waislamu kusherehekea Siku Kuu ya Idd-ul-Fitr.

Siku Kuu hii ni ya kuadhamisha mwisho wa mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

“Waziri wa Masuala ya Ndani Fred Matiang’i ametangaza rasmi Mei 3, kuwa siku ya mapumziko, siku ambayo wanafunzi wa kidato cha kwanza walitarajiwa kuripoti shuleni.

“Kwa sababu hiyo imeamulikwa kwamba siku ya wanafunzi hao kuripoti itakuwa Alhamisi, Mei 4, 2022. Tafadhali hakikisha kuwa mabadiliko haya yanazingatiwa,” Dkt Jwan akasema katika taarifa hiyo.

AJALI YAUA WATU 8 NA KUJERUHI 19

16:37 By






 


AJALI YAUA WATU 8 NA KUJERUHI 19


Watu wanane wamefarikia dunia na wengine 19 wamejeruhiwa katika ajali ya gari (Coaster T 287 CCY) mali ya Kanisa Katoliki Njombe iliyogongana na lori la makaa ya mawe, RPC Njombe, Hamis Issah amethibitisha.


WAZIRI MKUU MAJALIWA AONGOZA WAOMBOLEZAJI KUPOKEA MWILI WA MBUNGE WA VITI MAALUM

16:29 By


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo Aprili 27, 2022 amewaongoza waombolezaji kupokea mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Rukwa, Irene Ndyamkama kwenye uwanja wa Ndege wa Dodoma. Mheshimiwa Spika Dkt. Tulia Ackson (kulia kwa Waziri Mkuu) pia alishiriki katika mapokezi ya mwiili wa Mbunge huyo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo Aprili 27, 2022 amewaongoza waombolezaji kupokea mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Rukwa, Irene Ndyamkama kwenye uwanja wa Ndege wa Dodoma. Mheshimiwa Spika Dkt. Tulia Ackson (wa pili kulia) pia alishiriki katika mapokezi ya miili wa Mbunge huyo. 

Katibu wa Bunge, Mhe. Nenelwa Mwihambi, ndc akishiriki zoezi la kuuga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Rukwa, Mhe. Irene Alex Ndyamkama leo Aprili 27, 2022 katika viwanja vya Bunge Jijini Dodoma.

(PICHA NA OFISI YA BUNGE)